print-logo2
A+ A-

Injili ya Yesu | Gospel in Swahili

pdf

Ujumbe wa Injili

–  Tafadhali soma yafuatayo:

Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi
Warumi 3:23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu
Yohana 8:34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi

Mungu alituumba lakini hatumjui na tumetenganishwa na Yeye kwa sababu ya hali yetu ya dhambi. Maisha yetu bila Mungu hayana maana yoyote na lengo lolote. Matokeo (gharama ya malipo) ya dhambi zetu ni mauti, ya kiroho na ya kimwili. Mauti ya kiroho humaanisha kwamba tumetenganishwa na Mungu. Mauti ya kimwili ni kuoza kwa mwili. Tukikufa katika dhambi zetu tutatenganishwa milele na Mungu na kuishia jehanamu. Tunawezaje kujiokoa wenyewe kutokana na dhambi zetu na tumrudie Mungu? Hatuwezi kujiokoa kwa sababu haiwezekani kwa mtu mwenye dhambi kujiokoa (kama vile mtu anayezama hawezi kujiokoa mwenyewe). Wengine pia hawawezi kutuokoa kwa sababu sisi wote ni wenye dhambi (mtu mmoja anayezama hawezi kumwokoa mtu mwingine anayezama, wote wanahitaji msaada). Tunamhitaji yule asiyekuwa na dhambi (asiyekuwa anazama) ili atuokoe kutokana na dhambi zetu. Mtu asiyekuwa na dhambi tu ndiye anayeweza kutuokoa. Je, ni wapi utampata mtu asiyekuwa na dhambi katika ulimwengu wenye dhambi ambapo sisi wote ni wenye dhambi?

Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
Mathayo 1:23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi
Yohana 8:23 Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu
Marko 1:11 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe
Yohana 8:36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli
Yohana 3:3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Mungu, aliyetuumba na anayetupenda sana, alitupatia suluhisho. Kutokana na upendo Wake mwingi kwetu Alimtuma Mwanawe, Yesu, ili kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu hana dhambi kwa sababu Yeye hajatoka ulimwenguni, na, alipokuwa duniani, alishida majaribu ya shetani ya kutenda dhambi. Maisha yake yalimpendeza Mungu mbinguni. Yesu alibeba dhambi zetu na akafa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ni mkombozi wa maisha yetu (Yesu anaweza kutuokoa kwa sababu hakuwa anazama). Lengo la Yesu kufa msalabani ni kulipia gharama ya dhambi zetu na, kwa hivyo, kuondoa dhambi zetu kutoka kwetu na kurejesha uhusiano wetu uliovunjika na Mungu. Tunafufuka kutokana na mauti ya kiroho (kutengwa na Mungu) kupitia uwezo wa Mungu. Uhusiano huu mpya unaitwa kuzaliwa mara ya pili. Hii huturejesha kwa lengo letu la kuumbwa na kuwepo na, hutupa umaana na lengo la kweli la kuishi.

Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi
Warumi 6:9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena
Matendo ya Mitume 2:24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao
Warumi 14:9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia
Matendo ya Mitume 1:11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni

Je, kuna ushahidi gani kwamba dhabihu ya Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zetu ilikubaliwa na Mungu mbinguni? Ushahidi ni kufufuka kwa Yesu kutoka kwa mauti na Mungu. Kwa kufufuka, imedhibitishwa kwamba Yesu ameshinda mauti (au, kwa maneno mengine, mauti haina nguvu yoyote Kwake). Sasa, kwa hivyo, kwa sababu Yesu yu hai, tunaweza pia kuishi. Maisha yake ndani yetu hutupa maisha.  Pia, kwa sababu alifufuka, Yuko hai leo.

Yohana 5:24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani
Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho
Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi
Yohana 8:24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu
Matendo ya Mitume 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo
Warumi 10:13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka
Warumi 10:11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu
Warumi 3:22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti
Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka

Dhambi zetu zinawezaje kuondolewa na tupokee maisha haya mapya? Kwa kumwamini Yesu kama Bwana na Mkombozi wetu.  Tukitubu dhambi zetu na tumwombe Yesu atusamehe na atuokoe, atafanya hivyo. Yesu ni Mwana wa Mungu aliyekuja duniani kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Mtu yeyote duniani anayeweka imani yake Kwake atapokea msamaha kutoka kwa Mungu, ataokolewa kutokana na dhambi zao (na jehanamu) na atapokea maisha mapya kutoka kwa Mungu. Mungu haonyeshi upendeleo wowote. Yeye haathiriwi na – nchi unayoishi, lugha unayoongea, tajiri au maskini, mwanamume au mwanamke, kijana au mzee, au tofauti zingine za kimwili.  Kila mtu anayeamini na kukiri Yesu ataokolewa.  Ifuatayo ni maombi ambayo unaweza kuomba ukiamua kumfuata Yesu:

Mungu aliye mbinguni, asante kwa kumtuma Mwanawe wa kipekee, Yesu, ili afe kwa ajili ya dhambi zetu ili tuweze kuokolewa na kupata maisha mapya kutoka mbinguni. Ninatubu njia zangu na kuomba msamaha kwa dhambi zangu. Ninamwamini Yesu na ninampokea Yesu kama Bwana na Mkombozi wangu. Nisaidie na uniongoze ili niishi maisha yanayokupendeza katika maisha haya mapya ambayo utanipa. Amina.

Ukiwa umeomba maombi yaliyo hapa juu, mwombe Mungu akuonyeshe kanisa la kwenda. Ongea na Mungu kwa maombi mara kwa mara na Mungu ataongea na wewe. Sikiliza sauti ya Mungu. Mungu atakuongoza. Anakupenda na atakujali. Unaweza kumwamini. Hawaangushi wale ambao wanamwamini. Mungu ni Mungu mwema. Anaweza kuaminika. Unaweza kumtegemea kwa maisha yako. Leta mahitaji yako mbele Yake. Anakujali na atakubariki. Mungu alisema, ‘Sitakuwacha wala kukusahau’. Mwamini Mungu. Barikiwa na Yesu.

Soma biblia mara kwa mara, kuanzia kitabu cha Yohana. Kwa nyenzo zaidi za tovuti, bofya hapa.

SUV Biblia